(ABNA24.com) Wabunge wa Afghanistan wametoa mwito huo katika kikao cha jana cha bunge na kutangaza kuwa, kukutana Ashraf Ghani na Trump katika kituo cha anga cha Bagram kumeumiza hisia za wananchi wa nchi hiyo.
Katika kikao hicho, wabunge kadhaa wametangaza kuwa, hatua ya Rais Ashraf Ghani ya kwenda kituo cha kijeshi cha Bagram kwa ajili ya kukutana na Rais wa Marekani imeutia doa uhuru na kujitawala kwa Afghanistan na ni tusi kwa watu wa nchi hiyo.
Akihutubia kikao hicho cha Bunge, Balqis Roushan, mbunge wa mkoa wa Farah amesema: "Wamarekani wanahisi hawahitaji viza kwa ajili ya kuingia Afghanistan, na wakati wowote ule watakapo wanaingia nchini humu na kuwaita viongozi wetu wa kisiasa wakaonane nao; huu ni uhuru na kujitawala gani?"
Siku ya Alkhamisi ya tarehe 28 Novemba, Rais Donald Trump wa Marekani alifanya safari ambayo haikutangazwa nchini Afghanistan na kuelekea moja kwa moja kituo cha jeshi la anga cha Bagram waliko askari wa nchi yake katika ardhi ya Afghanistan. Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan na kaimu waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Asadullah Khalid walimfuata Trump na kwenda kuonana naye katika kituo hicho.
Safari hiyo ya Trump nchini Afghanistan na hatua ya Rais Ashraf Ghani ya kwenda kukutana naye katika kituo cha kijeshi cha Bagram vimekosolewa vikali na fikra za waliowengi, vyombo vya habari, wanasiasa pamoja na shakhsia mashuhuri wa Afghanistan.
..........
340